Diego Costa atafiti vilivyo ndani ya kikosi cha Paris Saint-Germain iwapo ataamua kuonda Chelsea majira ya kiangazi, hiyo ni kwa mujibu wa beki wa zamani wa Chelsea David Luiz.

Costa ambaye alifunga katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Everton ulioisha kwa sare ya 3-3, amekuwa akihusishwa na safari ya kurejea timu yake ya zamani Atletico Madrid.

Lakini Luiz anayekipiga na PSG tangu alipoondoka Stamford Bridge mwaka 2014, anaamini kuwa  Paris Saint-Germain miamba ya Ligue 1 (Ligi Kuu ya Ufaransa) itakuwa sahihi kwa Diego Costa.

“Diego Costa ni mmoja wa washambuliaji bora kabisa barani Ulaya, hakuna timu ambayo haitapenda kuwa nae,” alisema Luiz beki wa kimataifa wa Brazil.

“Nadhani PSG imeonyesha wazi ndani misimu mitatu au minne  iliyopita kuwa inasajili wachezaji waliobora kabisa. kama Dieogo atakuwa ametosheka na maisha ya England na anataka changamoto mpya, basi PSG ni sehemu sahihi kwake na atakaribishwa kwa moyo mkunjufu,” aliongeza Luiz katika maongezi yake na gazeti la Mirror la Uingereza.

Mtibwa Sugar Watuma Salamu Kwa African Sports
Picha: Msimu Mpya wa The Playlist ya Times Fm wazinduliwa kwa kishindo