Mahakama ya Wilaya ya Ilala leo imefutilia mbali mashtaka mawili ya ubakaji yaliyokuwa yanamkabili muimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel Mbasha.

Mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo leo iliyosomwa na na Hakimu Mkazi Flora Mujaya, baada ya kukamilisha utaratibu wa kusikiliza upande wa mashtaka pamoja na utetezi wa upande wa mshitakiwa, wiki mbili zilizopita.

Mbasha alikuwa akikabiliwa na mashataka mawili ya kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Katika shitaka ya kwanza, mbasha alidaiwa kumbaka shemeji yake huyo Mei 23, 2014 katika eneo la Tabata, Kimanga. Na katika shitaka la pili, Mwimbaji huyo wa nyimbo za injili anadaiwa kumbaka shemeji yake huyo ndani ya gari aina ya Toyota Ipsum.

Ilidaiwa kuwa Mbasha alifanya vitendo hivyo wakati ambapo alikuwa na matatizo na mkewe Flora, akimtuhumu kuisaliti ndoa yao.

Sumaye Aeleza Atakuwa ‘Nani’ Baada Ya Uchaguzi Mkuu
Graham Poll: Diego Costa Anastahili Adhabu