Uongozi wa Simba SC umetangaza kuwa Hamasa za kuelekea mchezo wa Mzunguuko watano wa Kundi C, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika zitazinduliwa Rasmi Keshokutwa Jumatano (Machi 15) katika eneo la Chanika Msumbiji.

Simba SC inajiandaa na mchezo huo utakaopigwa Jumamosi (Machi 18) katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, ikiwa na matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi ambao utaivusha kuelekea Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu 2022/23.

Ahmed Ally amethibitisha taarifa za kuanza kwa Hamasa kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC alipozungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatatu (Machi 13) jijini Dar es salaam.

“Kauli mbiu yetu kuelekea mchezo huu ni TUNAITAKA ROBO FAINALI.”

“Hamasa safari hii ni tunataka kujaza Uwanja wa Mkapa, tutapita kila eneo kuhakikisha hakuna Mwanasimba anabaki nyumbani siku hiyo. Tayari tumeanza kuona matawi kutoka mikoani yakipanga kuja Dar.”

“Hamasa yetu tutazindulia Msumbuji, Chanika Msumbiji ambapo wenyeji wetu litakuwa tawi la Simba Chanika Msumbiji na tutaanza saa 5 asubuhi. Balaa letu litaanzia Pugu Mnadani. Nayaalika matawi yote pamoja na ndugu zetu wanahabari.”

“Hawa Horoya pamoja na ukubwa wao wote tukiwapigia kelele hakuna namna wanaweza kutoka. Hawajazoea kucheza kwenye mazingira magumu ambayo tutawaonyesha siku hiyo. Ukiweza jichanganye kabisa ukiwa unakuja uwanjani.” Amesema Ahmed Ally

Simba SC inakwenda kwenye mchezo huo ikiwa imejikusanyia alama 06 zinazoiweka kwenye nafasi ya Pili katika msimamo wa Kundi C, ikitanguliwa na Raja Casablanca ya Morocco iliyokusanya alama 12 baada ya kushinda michezo mine waliocheza hadi sasa.

Hoyora AC inashika nafasi ya tatu katika Kundi hilo ikiwa na alama 04 baada ya kucheza michezo minne, huku Vipers SC ya Uganda ikiburuza mkia kwa kuwa na alama moja.

Young Africans kuivaa US Monastir kivingine
Simba SC yaanza kuiwinda Horoya AC