Marekani imeahidi kuwekeza na kuimarisha sekta ya afya pamoja na kuanzisha program ya kusaidia vijana wa Kitanzania kwa kuwajengea uwezo, ujuzi na maarifa ili kukuza maarifa yao pamoja na ajira.

Aidha imeahidi pia kushirikiana na Tanzania kukuza mitaji na kuvutia uwekezaji kutoka nchini humo ili kuchochea zaidi uchumi na huduma za kijamii hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Don Wright, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ofisini kwake Jijini Dodoma.

“Uhusiano wa Tanzania na Marekani ni imara na umedumu kwa zaidi ya miaka 60 sasa, ni wajibu wangu kuendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano huu kwa kuwahamasisha wawekezaji wengi zaidi kutoka Marekani kuja kuwekeza teknolojia na mitaji yao hapa nchini,” Amesema Dkt. Wright.

Naye Waziri wa Fedha na Mipango, Nchemba amesema Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara hapa nchini.

Aidha Dkt. Nchemba ameishukuru Marekani kwa kudhamiria kuleta program ya kusaidia kundi hilo kwa kutengeneza taasisi zinazoweza kuwaandaa vijana kujiajiri, jambo linalowakabili wahitimu wengi.

Dodoma itaendelea kuwa makao makuu ya nchi - Majaliwa
Mdee aibua mapya madeni ya mifuko ya hifadhi

Comments

comments