Muigizaji wa filamu za Kiswahili, Vicent Kigosi maarufu kama Ray amewataka wasanii wenzake kuwa makini na siasa ili wasitumiwe na kuachwa kama bazooka.

Ray ametoa mtazamo wake kupitia Instagram akiwataka wasanii hao kutokubali kutumiwa na wanasiasa katika kipindi hiki cha uchaguzi.

“Wasanii tuwe makini sana na campaign za siasa za mwaka huu tusitumike kama bigijii watutafune halafau watuteme kama big jii watutafune halafa watuteme, tuwe makini kumsapoti mgombea atakayesaidia tasnia ili maisha yetu yasongee hata kumi mbele. Utabaki kuwa ni mtazamo wangu tu wasnii tuamke kutetea maslahi yetu wakati ndio huu,” aliandika Ray.

Azam FC Yashinda Mchezo Wa 10 Mfululizo
Dk. Slaa Kuondoka Nchini, Asisitiza Hajawahi Kuwa Na Akaunti Twitter