Msanii nguli wa uigizaji nchini, Bongo Movie, Jacob Steven maarufu kwa jina la ‘JB’ amesema kuwa yuko mbioni kuachana na suala la uigizaji, hivyo kuelekeza nguvu zake katika suala zima la kuwa mtayarishaji wa filamu.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki katika shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na Kampuni ya Startime, ambapo amesema kuwa katika fani hiyo ya uigizaji wa filamu ameitumikia kwa muda mrefu hivyo ameamua kuwa mtayarishaji wa filamu hizo.

“Mimi nina miaka ishirini katika fani hii, ni lazima nijikite katika kitu kimoja ambacho kitakuwa cha kipekee, hivyo kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja itaniwia ugumu kulingana na umri wangu, ingawa nitaendelea kuzitengeneza lakini sitaigiza,”amesema JB

Video: Cassper Nyovest aachia ngoma mpya, yumo Vanessa Mdee
Chelsea, Barcelona, Man Utd kibaruani leo