Marudio ya kura za maoni katika baadhi ya majimbo ili kuwapata wagombewa watakaogombea nafasi za ubunge kwa tiketi ya CCM yamekamilika huku yakimtupa nje ya Bunge, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.

Dk. Seif amelazimika kuliachia jimbo la Rufiji baada ya kushindwa katika kura za maoni na mpinzani wake anaefahamika kwa jina la Mohamed Mchengelwa.

Dk. Seif anaongeza idadi ya mawaziri takribani sita walioangushwa katika kinyang’anyiro cha kura za maoni.

seif

Katika hatua nyingine, Meya wa Ilala anayemaliza muda wake, Jerry Slaa ameibuka mshindi katika marudio ya kura za maoni, hivyo kumpa nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya ubunge kama ilivyokuwa ndoto yake.

“Mambo hadharani…… Nawashukuru wote,” Jerry Slaa ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

Sakata La Mourinho Na Daktari Wake Lapiga Hatua
Harakati Za Usajili Barani Ulaya