Serikali kupitia Wizara ya Elimu, imesema zaidi ya programu 300 za mafunzo elimu ya juu zinatarajia kuanzishwa ama kuhuishwa, ili kuendana na dira, mipango ya Maendeleo ya Taifa na mahitaji ya sasa ya kijamii, kiuchumi na soko la ajira.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum, Nusrati Shaaban Hanje aliyetaka kujua ni lini Serikali itapitia mitaala ya Vyuo Vikuu, ili kufungamanisha elimu na dira na mipango ya maendeleo ya Taifa.

Amesema, tayari Vyuo Vikuu vya Serikali na Binafsi kupitia mradi wa ‘Higher Education for Economic Transformation – HEET,’ vimepata mafunzo mbalimbali ya kuandaa programu zinazoendana na vipaumbele vya nchi na mahitaji ya soko la ajira.

Aidha, Prof. Mkenda ameongeza kuwa katika kutekeleza hilo Vyuo vimeunda Kamati za Ushauri wa Insia (Industrial Advisory Committees -IACs) zenye wajumbe kutoka Sekta za Waajiri kwa ajili ya kutoa ushauri kwa taasisi hizo juu ya programu zinazoendana na soko la ajira.

Rasmi Sadio Mane anasepa Bayern Munich
Axel Disasi kutua Manchester United