Kiungo kutoka nchini Hispania Sergio Busquets Burgos ameingia kwenye rekodi mpya za FC Barcelona, kufuatia kucheza michezo zaidi ya 500, tangu alipopandishwa kwenye kikosi cha kwanza mwaka 2008.

Busquets mwenye umri wa miaka 32 ameingia kwenye rekodi hiyo, baada ya kufikisha idadi ya michezo 594, aliyocheza klabuni hapo, huku akimshusha beki na nahodha wa zamani wa Barca Carles Puyol katika nafasi ya nne kwa wachezaji walioichezea Barcelona michezo mingi zaidi katika historia ya klabu hiyo.

Kiungo huyo alifikisha idadi hiyo ya michezo alipokuwa sehemu ya kikosi cha FC Barcelona kilichepambana dhidi ya Real Sociedad walioshinda mabao mawili kwa moja.

Miongoni mwa michezo 594 ya Busquets, imetokana na ushiriki wake kwenye michuano michuano sita duniani. michezo 390 ya Ligi ya Hispania (La Liga), 117 Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, 64 Kombe la Mfalme (Copa del Rey), 15 Spanish Super Cup, 5 Klabu Bingwa duniani (Club World Cup) na 3 European Super Cup.

Mchezaji huyo alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na miaka 20 mwaka 2008/09, chini ya meneja Pep Guardiola dhidi ya Racing September 13 na FC Barcelona walifanikiwa kuchukua mataji matatu (treble) katika msimu huo.

Wanaoongoza kwenye orodha ya wachezaji waliochezwa michezo mingi wakiwa na FC Barcelona: 1. Xavi Hernandez (767), 2. Lionel Messi(747), 3. Andreas Iniesta (674), 4. Sergio Busquets (594) na 5. Carles Puyol (593).

Waamuzi 17 Tanzania watambuliwa FIFA
Deogratius Munish ‘Dida’ arudi Ligi Kuu