Rais mteule wa Nigeria, Asiwaju Bola Tinubu ameelezea hofu yake kuhusu njama za baadhi ya wapinzani wake aliowashinda katika uchaguzi Mkuu kutaka kusitisha mchakato wa mpito na maandalizi ya kuapishwa kwake rasmi Mei 29, 2023.

Tinubu katika taarifa ya Mkurugenzi wake, Masuala ya Umma na Waziri wa Nchi Kazi na Ajira, Festus Keyamo amewaonya wapinzani wa Peoples Democratic Party PDP, Alhaji Atiku Abubakar na wa Labour Party LP, Peter Obi kuacha malalamiko na kufuatilia kesi zao mahakamani.

Amesema, Viongozi hao wameingia barabarani kupinga utawala wake na wamedhamiria kupata haki ya kuwa na Serikali ya umoja wa Kitaifa, lakini wanapaswa kuelewa kuwa Tinubu ni Rais wa Nigeria na hotuba zake za hadhara na matamshi yake yamejikita katika upatanisho, msamaha na maono makubwa kwa Wanigeria.

Rais mteule wa Nigeria, Asiwaju Bola Tinubu. Picha ya Vanguard.

“Kwa sababu wanazozijua wao, watu hawa wamekaa na hasira eti kwanini Asiwaju Bola Ahmed Tinubu alitangazwa mshindi wa uchaguzi Mkuu wa 2023, lakini kwa bahati mbaya watu hawa wapotofu wametaka ama kufutwa kwa matokeo au kwamba Rais Mteule asiapishwe tarehe 29 Mei, 2023,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Hata hivyo, ilibainishwa kuwa, Rais Mteule anawafahamu wanaofadhili maandamano yenye vurugu dhidi ya mamlaka yake, wanaoishi ndani na nje ya Nigeria na atashirikiana kwa karibu na vyombo vya usalama, ili kuwakamata na kuwafikisha mahakamani.

Taifa Srats Vs The Cranes kupigwa saa mbili usiku
Mo Farah kukiwasha Port-Gentil Marathon