Idara ya maendeleo ya kimataifa ya Marekani – USAID, imesema inasitisha msaada wa chakula kwa nchi ya Ethiopia kutokana na kutowafikia walengwa na uwepo wa tuhuma kuwa chakula kingine hupelekwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya USAID, imesema inatarajia kuona misaada hiyo ya chakula itatolewa tena kwa njia ya kuaminika na inayostahiki na kuwafikia walengwa, na kwamba bado haijagundulika ni nani aliye nyuma ya biashara ya vyakula vya msaada.

Msemaji wa Idara hiyo, ameeleza katika taarifa yake kwamba USAID imegundua kwa kushirikiana na serikali ya Ethiopia kuna uwepo wa kampeni iliyoenea na iliyoratibiwa ya msaada wa chakula kupelekwa sehemu nyingine na kutowafikia watu wa Ethiopia kama ilivyopangwa.

Zaidi ya watu milioni 20 wanahitaji chakula kutokana na ukame na vita vilivyomalizika hivi karibuni katika mkoa wa kaskazini wa Tigray na umetolewa baada ya tangazo la USAID na Program, ya Chakula ya Umoja wa Mataifa, WPF.

Rais Dkt. Mwinyi ashikiri Mkutano wa TNBC
Siku ya Mazingira: GGML yatoa elimu taka za plastiki