Beki mzawa Kennedy Juma amesaini mkataba mpya wa miaka miwili ndani ya klabu ya Simba.

Kennedy ambaye amekuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao, alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokua wanamalizamikataba yao mwishoni mwa msimu huu.

Leo mchana imethibitika rasmi kuwa, beki huyo ambaye alijiunga na Simba SC akitokea Singida United, amekamilisha mpango wa kusaini mkatana mpya ambao utaendelea kumuweka Msimbazi hadi mwaka 2023.

Kennedy alionesha uwezo mkubwa kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa Robo Fainali wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs Jumamosi (Mei 22) akichukuwa nafasi ya Joash Onyango aliepata majeraha ya kichwa kipindi cha kwanza.

Wakati huo huo taarifa kutoka ndani ya klabu yaSimba zinadai kuwa Mabosi wa simba wameendelea kuwaongezea mikataba wachezaji wao uongozi wa Klabu hiyo unaendelea kufanya mazungumzo na mlinda mlango chaguo Beno Kakolanya.

Hata hivyo inaelezwa kuwa pande hizo mbili zinaendelea kuvutana kuhusu upande wa masilahi.

UEFA yathibitisha Conference League
Rais wa Ufaransa kufanya ziara Rwanda