Maofisa wa Polisi katika kaunti ya Bungoma, Magharibi ya Kenya wamemtaka Mhubiri Ronald Nakalila Wanyama (Nabii Yohana), kujisalimisha kituoni kwa mahojiano Juni 2, 2023 kwa hiari yake.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi kaunti ya Bungoma, Francis Kooli, amesema mhubiri huyo atahojiwa kuhusu namna anavyoendesha shughuli za kanisa lake.

Nakalila Wanyama mwenye umri wa miaka 83, ni kiongozi wa kanisa la Church for All Nations lililopo Magharibi ya taifa hilo, amekuwa akisema anatarajia kuzindua Biblia yake na sarafu mpya.

Mhubiri huyo pia mwenye Wanawake 42 na watoto 289, anachunguzwa kutokana na mafunzo yake ya kidini yanayotiliwa shaka.

TFF yazikana shutuma zilizoelekezwa Young Africans
Hatma ya Minziro, Wandiba kujulikana leo