Mataifa ishirini na mbili yamefanikiwa kufuzu fainali za kombe la dunia 2018, zitakazochezwa nchini Urusi baada ya purukushani ya michezo ya kuwania tiketi hatua ya makundu iliyomalizika usiku wa kuamkia leo katika baadhi ya kanda zinazotambuliwa na FIFA.

Urusi ni taifa pekee lililoingiza timu yake ya katika fainali hizo, kwa kigezo cha kuwa mwenyeji na kufikisha idadi ya timu 22, ambazo zinasubiri kupangwa katika makundi ya kushiriki fainali hizo.

Kimahesabu bado mataifa kumi ili kukamilisha idadi ya mataifa Thelathini Na Mbili ambayo kikanuni yanapaswa kushirii fainali za kombe la dunia.

Mataifa yaliyosalia yatapatikana kwa michezo ya hatua ya mtoano kwa baadhi ya kanda ikilitoa bara la Afrika, na hii ni kwa mujibu wa kanuni za michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia.

Mpaka sasa mataifa yaliyofuzu kutoka Ukanda wa Ulaya ni, Ubelgiji, England, Ufaransa, Ujerumani, Iceland, Poland, Ureno, Urusi (Mwenyeji), Serbia na Hispania.

Amerika ya kusini:

Brazil, Uruguay, Argentina na Colombia

Afrika:

Misri na Nigeria

Asia:

Iran, Japan, Saudi Arabia na Korea kusini

Amerika ya kaskazini, kati na Caribbean

Costa Rica, Mexico na Panama

Polisi Dar wasambaratisha mkutano wa Sheikh Ponda
Sadio Mane kurejea uwanjani mwezi disemba