Msanii pekee wa Tanzania aliyefanya kazi na Akon baada ya kushinda shindano la Airtel Trace Music, Mayunga huenda akamuandikia shairi la Kiswahili msanii huyo katika wimbo wa pili watakaofanya pamoja.

Afunguka katika kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm, Mayunga ambaye kazi yake ya ‘Please Don’t Go Away’ aliyofanya na Akon inafanya vizuri, alieleza mpango huo wakati akieleza sababu za kukosekana kwa verse ya Akon kwenye wimbo wake kama ilivyokuwa ikitarajiwa na wengi.

Mayunga alieleza kuwa baada ya kukamilisha kuimba wimbo huo ulioandikwa na Akon mwenyewe, [Akon] aliusikiliza na kueleza kuwa haoni sehemu ya yeye kuimba kwakuwa wimbo ulikuwa mkali tayari. Hivyo, akatoa wazo la kufanya wimbo mwingine ambao Manyunga atamuandikia verse ya Kiswahili na kumsaidia kuiimba kwakuwa hajui lugha hiyo.

Msanii huyo aliridhia wazo la Akon na kukamilisha wimbo huo ambao ni sehemu ya zawadi aliyopewa baada ya kushinda shindano la Airtel Trace Music.

Katika hatua nyingine, Mayunga ambaye alikuwa chini ya Label ya Universal Music, alieleza kuwa aliamua kuvunja mkataba wa label hiyo baada ya kuona haitekelezi makubaliano ya kuusogeza muziki wake kwa wakati, hivyo sasa anasimamiwa na Trace.

 

Serengeti Boys Kurejea Nyumbani Hii Leo
Kitambi Aelezea Kilichoitafuna Azam FC Dhidi Ya Young Africans