Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka viongozi na watendaji wote wa sekta ya maji nchini kufanya kazi kwa uzalendo, bidii na weledi na kwa kutanguliza maslahi mapana ya nchi, ili kufikia malengo ya kufikisha maji kwa kiwango cha asilimia 85 Vijijini na asilimia 95 Mijini ifikapo mwaka 2025.

Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa watendaji wa sekta ya maji uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma, amesema Tayari, miradi 67 imekamilika kwa gharama ya shilingi bilioni 759.211 na utekelezaji wa miradi 110 ipo katika hatua nzuri za uendelezaji.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa, amewahasa watendaji wa sekta maji nchini kushirikiana na wanajiosayansi kufanya tafiti za mara kwa mara zitakazowezesha kuwa na takwimu za uhakika kuhusu kiwango cha maji, mahali yalipo na ujazo wake.

“Kama nilivyotangulia kueleza kuwa maji ni chachu katika maendeleo ya viwanda nchini. Kwa mantiki hiyo, uwepo wa takwimu sahihi kuhusu upatikanaji wa maji ni muhimu katika kurahisisha na kuvutia uwekezaji wa viwanda kote nchini”

Waziri Mkuu ameigiza Wizara ya Maji ishirikiane na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kusimamia vema na kwa uadilifu rasilimali fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji ili miradi iweze kukamilika kwa wakati na uwepo wa thamani ya fedha za walipa kodi.

Sambamba na hayo Majaliwa amekabidhi pikipiki 147 kwa ajili ya mameneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Viijini, malori matatu ya kunyonya majitaka kwa halmashauri za miji ya Kahama, Tanga na Lindi.

Elimu ya hakimiliki itolewe kwa wabunifu- Majaliwa
Roketi zapiga mji wa Tel Aviv baada ya ghorofa kuharibiwa Gaza