Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula, amesema kuwa Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi atawasili kesho Tanzania Juni 9, 2021.

Amesema kuwa ujioo wa Rais Masisi Tanzania, lengo ni kukuza uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.

Ameeleza kuwa Rais Masisi atakuwa Tanzaniakwa ziara ya siku mbili ya kikazi kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

“Mfululizo wa ziara hizi ni kukuza na kuimarisha diplomasia za kiuchumi kutoka kwa wenzetu” amesema Balozi Mulamula.

Karia apata mpinzani TFF
Muuaji wa halaiki afungwa kifungo cha maisha