Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20  imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sudan katika mchezo wa nusu fainali ya michunao ya CECAFA  huko Uganda.

Mabao ya Tanzania yamefungwa na Israel Mwenda pamoja na Kelvin John huku la Sudan likiwekwa kimiani na Mohammed Abbas.

Matokeo hayo yanaifanya Tanzania itinge hatua ya fainali na sasa itakuwa na mshindi kati ya Kenya dhidi ya Eritrea ambao wanacheza hivi sasa.

Timu hiyo ya vijana ilifanikiwa kutinga hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kuifunga Uganda timu ambayo ni mwenyeji wa mashindano hayo kwa magoli 4-2.

Aidha kabla ya mchezo wa leo kocha mkuu wa timu hiyo Zuberi Katwila alisema atatumia muda wa dakika 10 ili kuwachunguza wapinzani wao na kujua mbinu ambazo kiufundi zitampa nafasi nzuri ya kubaini ubora na udhaifu wa timu ya Sudan.

Maabara 13 zafungiwa na zoezi kuendelea nchi nzima
Video: Anasumbuliwa na maradhi makubwa matatu, mwenyewe asimulia "Muda wowote nakufa, Mungu anaweza''