Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa Kocha Mkuu wa klabu ya Mbeya City inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Meja Mstaafu Abdul Mingange kufuatia kifo cha mke wake Fatma Juma kilichotokea mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

Katika salamu zake kwenda kwa familia ya marehemu, TFF imempa pole mme wa marehemu Meja Mingange, ndugu jamaa, marafiki pamoja na klabu ya Mbeya City kufuatia kifo hicho.

Mazishi ya marehemu Fatma Juma yamefanyika Jumapili iliyopita katika makaburi ya Matombo mkoani Morogoro.

Samir Nasri Kuongeza Nguvu Man City
Florentino Perez Azima Ndoto Za Wapinzani