Uongozi wa klabu ya Arsenal umekanusha taarifa za kumuwania meneja wa klabu ya Borussia Dortmund inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Ujerumani, Thomas Tuchel.

Juzi, klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London, iliripotiwa kuwa katika mipango ya kumrithisha mikoba ya Arsene Wenger meneja huyo, ambaye ameonyesha kuwa na umakini kubwa katika ukufunzi wake tangu alipokubali kupokea kijiti kutoka kwa Jurgen Klopp.

Arsenal wamekanusha kumfuatilia Tuchel, lakini bado wanaendelea kushikwa na kigugumizi kuhusu meneja wa mabingwa wa soka nchini Italia, Juventus aitwae Max Allegri ambaye kwa kipindi kirefu amekua akitajwa huenda akamrithi Arsene Wenger.

Kutokana na hatua hiyo, bado inaaminika kuwa Allegri huenda akawa chaguo la kwanza la viongozi wa Arsenal, endapo wataafiki kuachana na Arsene Wenger mwishoni mwa msimu huu, ambapo mkataba wake wa kukinoa kikosi cha The Gunners utakua unafikia kikomo.

Wawili Kuzaba Nafasi Ya Lukaku
Magazeti ya Tanzania leo Machi 22, 2017