Rais  Magufuli leo Oktoba 26, 2017 amefanya uteuzi wa Wakuu wa mikoa nchini kufuata baadhi ya Wakuu wa Mikoa kustaafu, katika watu walioteuliwa na Rais miongoni mwao ni aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti, Dkt Adam Malima.

Akizungumza kwa niaba ya Rais, Ikulu leo Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Balozi John William Herbert Kijazi amewataja wakuu hao wa mikoa walioteuliwa na wengine kubadilisha vituo vya kazi kuwa ni pamoja na.

Mkoa wa Manyara – Alexander Mnyeti

Mkoa wa Rukwa   – Joakim Wangabo

Mkoa wa Geita   – Robert Gabriel

Mkoa wa Mara    – Adam Kighoma Malima

Mkoa wa Dodoma  – Bi. Cristin Mdeme

Mkoa wa Mtwara  – Gelasius Byakanwa

Video: Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam zaleta maafa
Msando apata shavu serikalini