Viongozi wa Kiserikali na Wafanyabiashara mashuhuri barani Afrika, wanatarajia kukutana kwa siku tatu nchini Ghana mwishoni mwa mwezi huu kujadili na kuunda jukwaa la kila mwaka, la kiuchumi.

Mkutano huo, umethibitishwa rasmi kufanyika kwake na Ofisi ya Rais wa Ghana, Nana Addo Akufo-Addo na ile ya Katibu Mkuu wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA), Wamkele Mene.

Aidha, inaarifiwa kuwa Mkutano huo uliopangwa kufanyika Januari 26 hadi 28, 2023 utakuwa wa kwanza wa msururu wa mazungumzo na mpango wa mtandao na mustakabali wa Afrika (APN).

Taarifa ya Katibu Mkuu wa AfCFTA imesema, “Mkutano huu utawaleta pamoja viongozi wa kisiasa na kibiashara barani Afrika, pamoja na viongozi wengine wenye mawazo kuhusu Afrika.”

Aidha, taarifa hiyo pia imeeleza kuwa watajadiliana kuhusu mradi muhimu wa soko moja la Afrika, lakini pia kuundwa kwa jukwaa la kila mwaka kwa viongozi wa bara hilo ili kuongoza utekelezaji shirikishi wa Mkataba wa Biashara Huria wa Bara la Afrika.

Simba SC, Makusu mambo yamenyooka
Young Africans yatangaza vita ya kisasi