Mshambuliaji wa klabu ya VfB Stuttgart Silas Wamangituka ameuambia uongozi wa timu hiyo kuwa hilo sio jina lake halisi.

Mshambuliaji huyo ambaye ndiye kinara wa mabao wa timu hiyo katika msimu uliomalizika amesema jina hilo lilibadilishwa na wakala wake wa zamani aliyekuwa akihangaika kuhakikisha anatimiza ndoto yake ya kucheza soka akiwa na umri mdogo.

Silas amesema ameamua kuweka wazi kwakuwa amekuwa akiishi kwa wasiwasi bila uhuru tangu alipoondoka CONGO DR Congo akiwa na umri wa miaka 17.

“Ni ngumu kwangu kuielezea stori hii lakini imebidi niseme kutokana na ushauri wa washauri wangu, jina langu halisi ni Silas Katompa Mvumpa” Amesema Silas

Katika hatua nyingine Silas amesema alibadilishiwa hadi mwaka wa kuzaliwa na kuweka 1999 wakati uhalisia wake alizaliwa mwaka 1998

Kwa upande wa Stuttgart kupitia kwa Mkurugenzi wao wa michezo Thomas Hitzlsperger wamesema watalifuatilia suala hilo kwa kina kwa kushirikiana na mamlaka husika ili kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufafanuzi zaidi.

Chanzo Yanga kumkataa Ajibu chaanikwa
Tarimba Abbas: Wengi wananishawishi kugombea Urais TFF