Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watuhumiwa wawili Shine Ngula (23), mkulima wa Mawemilu Tarafa ya Nindo Wilaya ya Shinyanga vijijini na Kisinza Lusamila(28), mkulima wa mpanda mkoani Katavi kwa kosa la mauaji ya Hadija Kisinza (60).

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Mjini Kahama, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba amesema mara baada ya tukio hilo kutokea upelelezi ulifanyika na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao huko Mpanda Mkoani Katavi ingawa bado wanaendelea na upelelezi.

Aidha watuhumiwa hao wamekiri kufanya kosa hilo na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakani kujibu tuhuma inayowakabili.

Kamanda Magiligimba amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia msako mkali unaoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga wa kupambana na uhalifu na wahalifu.


Aidha Kamanda Magiligimba ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa juu ya watuhumiwa wengine waliohusika kwenye tukio hili na kuwataka watuhumiwa kujisalimisha wenyewe kwani watakamatwa tu.

Jaji Warioba: Ajira za Serikalini hazitoshi
Macron akiri Ufaransa kuhusika na mauaji ya kimbari Rwanda