Rais mteule wa Marekani, Donald Trump amesema yuko tayari kuanza kuwasafirisha makwao wahamiaji haramu milioni tatu kutoka Marekani baada ya kuapishwa kuwa rais wa nchi hiyo.
Trump amesema wahamiaji wote wenye rekodi za uhalifu, ikiwemo makundi ya wahalifu na wauza dawa za kulevya ndio watakuwa kipaumbele chake cha kwanza kuwarudisha makwao, ameongeza kuwa sehemu ya ukuta ambao aliahidi kujenga kwenye mpaka baina ya nchi yake na Mexico, utakuwa ni uzio wa kuzuia wahamiaji hao haramu.