Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imemzawadia Rais Mstaafu wa Pili, Ali Hassan Mwinyi gari jipya aina ya Mercedes Benz ili kumsaidia kufanya shughuli zake, kwani gari la awali lilikuwa juu saa hivyo kumpa changamoto wakati wa kupanda na kushuka.

Akizungumza Leo Mei 8, wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Mzee Mwinyi “Safari ya Maisha yangu Mzee Ruksa” Rais Samia amesema kuwa Mzee mwinyi amekuwa akipata sana usumbufu kwenye lake awali wakati wa kupanda na kushuka kutokana na kimo cha Mzee Mwinyi na Hivyo kuamua kumzawadia gari hilo.

Aidha Rais samia maesema kuwa serikali itaendelea mkutunza Mzee Mwinyi lakini pia maemshukuru kwa kumualika kuzindua kitabu hiko.

“Nakushukuru sana Mzee wangu Rais Mstaafu Mwinyi kwa kunikaribisha kuzindua kitabu cha simulizi ya maisha yako, nampongeza Mzee Mwinyi kwa kuamua kuandika kitabu ambacho sio tu kitawasaidia Watanzania na Dunia kumfahamu pia kina historia ya Tanzania,” Amesema Rais Samia.

Sambamba na hayo Rais Samia ameainisha mambo muhimu yakufunza yaliyo katika kitabu hicho ikiwemo kutambua kuwa uongozi unatoka kwa mungu, lakini pia uongozi ni dhamana, pia jambo kubwa kitabu hicho kinakumbusha kuwa binadamu hatuna budi kupendana na kuheshimiana na kutufundisha kutokuishi kwa visasi.

Sheikh auawa akiongoza ibada msikitini
Samia: Mzee Mwinyi ni Baba wa Mageuzi