Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa  Ibrahim Juma ameutaka uongozi mpya wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kuusoma na kuuelewa mpango mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania ili umoja huo uweze kuchangia katika kuutekeleza.
Ameyasema hayo mara baada ya kkutembelewa na uongozi wa  TLS ulioongozwa na Rais wa chama hicho,   Tundu Lissu.
Amesema ni vema kuusoma Mpango Mkakati huo  kufahamu ni wapi mahakama inatoka na wapi inapotaka kuelekea hususani  katika suala zima la maboresho ya huduma ya utoaji haki nchini.
Aidha, Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania (2015/2016-2019/2010) umegawanyika katika nguzo kuu tatu ambazo ni utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali.
Nyingine ni upatikanaji na utoaji haki kwa wakati na kurejesha imani ya jamii na ushirikishwaji wa wadau na umejikita katika kuboresha huduma za utoaji haki kwa ujumla.
Kwa upande wake Rais wa TLS, Tundu Lissu pamoja na mambo mengine  amesema kuwa kuna changamoto nyingi zinazo wakabili mawakili nchini .
Hata hivyo, amezitaja changamoto hizo ni  pamoja na baadhi ya mahakama kutokuwa na Ofisi kwa ajili ya mawakili, taratibu za usajili wa mawakili, na nyingine.

Babu Tale adai akipata matatizo chanzo ni Shigongo, asimulia maongezi yao
Jamii yatakiwa kubadilika, yahimizwa kutunza mazingira