Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgera kilichopo Wilaya na Mkoa wa Iringa, Lucas Mgata ametakiwa kujisalimisha kituo cha Polisi kutokana na tuhuma za uchochezi wa migogoro ya ardhi kwa wananchi wa Kijiji chake zinazomkabili.

Agizo la kujisalimisha kwa limetolewa na Mkuu wa wilaya ya Iringa, Mohamed Hassan Moyo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Kijiji hicho, na kusema mwenyekiti huyo amekiuka amri ya Serikali iliyositisha kwa muda ya matumizi ya ardhi ili kuchunguza madai ya wananchi kuporwa ardhi na kiongozi huyo.

Mkuu wa wilaya ya Iringa, Mohamed Hassan Moyo.

Mkuu wa Polisi wilaya ya Iringa, Mrakibu mwandamizi wa Polisi, Bernad Samara naye amsisitiza juu ya mwenyekiti huyo kujisalimisha kutokana na kukaidi amri ya serikali.

Mwenyekiti huyo, Lukasi mgara analalamikiwa na wananchi wa kijiji cha Mgera kupora maeneo ya wananchi ambapo sasa kamati ya ulinzi na usalama imepiga marufuku shughuli za kibinaadam katika eneo hilo ili kupisha uchunguzi.

Waziri Mkuu atoa maagizo kwa Wizara miradi ya maji
Rais samia aanza ziara Jamhuri ya watu wa China